Kerr wa gormahia yupo tayari kurejea simba kwa masharti haya

0
7Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, Dylan Kerr amesema yuko tayari kurejea Simba, lakini ametoa masharti.

Kerr amesema anaweza kurejea na kuifundisha Simba ikiwa kama rundo la viongozi waliopo sasa wataondolewa.

Kerr ameiambia SALEHJEMBE mjini Nakuru, Kenya kwamba aliamua kuondoka Simba kutokana na matatizo lukuki yaliyosababishwa na viongozi.

“Bado baadhi yao wapo, ni watu ambao wanaingilia kazi za makocha, hawajui wanalolifanya na hakuna kocha anayeweza kuja akafanikiwa.

“Simba ndiyo, naipenda na kama kurudi inawezekana. Lakini ni lazima uongozi wa sasa kama ni wamiliki, wawaondoe watu hao.”

Kerr ameiwezesha Gor Mahia kuchukua ubingwa wa Kombe la SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo, safari hii wakiifunga Simba kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here