Huenda Yanga ikaanza kuutumia uwanja wa kaunda msimu ujao

0
6

Licha ya changamoto lukuki za kiuchumi zilizoikumba klabu ya Yanga, lakini viongozi wake wanastahili pongezi kwa juhudi kubwa wanazofanya kuhakikisha timu hiyo inajitegemea kwenye baadhi ya mambo.


Wakati Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa anatangaza mikakati ya kuukarabati uwanja wa Kaunda ili uweze kutumika kwa ajili ya mazoezi na baadae ukikamilika uwe uwanja rasmi wa nyumbani wa Yanga, jambo hilo lilikuwa kama ndoto.

Wako waliokuwa wakibeza juhudi hizo zilizokuwa zikifanywa na viongozi kutokana na hali ya eneo la Jangwani, lakini mwanga umeanza kuonekana hasa baada ya zoezi la kujaza kifuzi uwanjani kukamilika.


Kwa ukarabati unaoendelea pale uwanja wa Kaunda upo uwezekano mkubwa msimu ujao Yanga ikaanza kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.


Kwa hili, yafaa tuwapongeze, juhudi zao zimeonekana na hakika zitazaa matunda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here