Hatimae lopetegui atimuliwa hispania ni kocha aliyetangazwa madrid

0
13

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania ,  Julen Lopetegui amefukuzwa kazi rasmi na shirikisho la soka nchini Hispania RFEF .

Kufukuzwa kwa kocha huyo kumekuja siku moja baada ya Kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Real madrid ya nchini hispania akichukua nafasi ya Zinedine zidane aliyejiuzuru siku chache zilizopita .

Swala hilo lilimkera sana raisi wa shirikisho la soka nchni Hispania bwana Luis Rubiales na kumpelekea kuitisha mkutano wa muda wa kuongea na Lopetegui Kwaajili ya Kupata muafaka .

Katika mkutano na waandishi wa habari raisi Rubiales amesema kwamba Lopetegui alifanya Uamuzi huo pasipo kuwashirikisha na wameamua Kumfukuza Kazi rasmi .

Kwa sasa kikosi cha timu hiyo ya taifa ya hispania kipo chini ya mkurugenzi wa ufundi wa timu ya taifa ya hispania ,  Fernando Hierro akisaidizana na Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Vijana ya nchi hiyo chini ya Umri wa miaka 21 bwana Alberto Celades .

Rjm Pilen

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here