Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani – TID

0
17

Msanii
TID amesema kuwa utaratibu wa wadau/media kushusha wasanii pale
wanapodai maslai yao na kuwapandisha wengine ndio kitu kinaathiri muziki
wa Bongo Flava.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa kitu hicho ndicho kilitokea kwenye muziki wake na kwa sasa kimemtokea Diamond.
“Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu
anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo
limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa,”
amesema.
“So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa
tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka
kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,” TID ameiambia Wasafi TV.
TID ameongeza kuwa hajaona kitu kama hicho nchini Kenya kwani bado
anamuona Jaguar ni msanii mkubwa, Nonini ni msanii mkubwa anapewa
heshima yake hakuna underground yeyote amewekwa pale kumshusha Nonini.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here