Baada ya kuchezea kichapo ulingoni hatimaye, David Haye atangaza kustaafu masumbwi

0
10

Mwanamasumbwi
bingwa wa Dunia, David Haye ametangaza kustaa mchezo huo hii leo ikiwa
imepita mwezi mmoja pekee tangu kupoteza pambano lake la marudiano dhidi
ya Tony Bellew ndani ya ulingo.

Bondia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 37, ameamua kutangaza
kuachana na ngumi baada ya mapambano yake 32 toka kuanza mchezo huo huku
akishindwa kufua dafu mbele ya Bellew mwezi mmoja uliyopita.

Akiwa ameanza mapambano ya kulipwa mwaka 2002, Haye amefanikiwa
kushinda michezo 28 huku akiwapiga watu kwa KO mara 26 na kupoteza minne
pekee kwa muda wote huo.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here