Aliyejitosa kwa Zari afunguka ‘Tunajua huwezi kurudiana na Diamond’

0
3


Msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya, Ringtone Apoko ameonyesha kuchukizwa na tetesi za Zari kurudiana na Diamond.

Utakumbuka hivi karibuni Ringtone alieleza hisia zake kuwa anataka
kumuoa Zari, alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa alishanunua gari aina
ya Range Rover Sport ya mwaka 2017 kwa ajili ya mrembo huyo.

Sasa Rington Apoko amesema atashangaa ikiwa Zari atarudi kwa Diamond
ingawa anajua hawezi kufanya hivyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram
ameandika;

Mpendwa Zari huwezi ukaendelea kusoma kurasa za kitabu
kile kile kila siku ilihali unajua kitakavyoishia, ulioandoka Misri
ukaenda Kanani itasikitisha kama utarudi tena.

Nini kitatokea kwa wasichana kibao uliowaambia sasa unamjenga Zari?
Ushauri wangu ni kuwa hivi sasa mtafute Mungu kwa kufunga na maombi ili
Mwenyezi Mungu akupe mwelekeo. Lakini hivi sasa hatuna wasiwasi maana
wote tunajua huwezi kurudiana na Diamond.

Muimbaj huyo amekuwa akituma jumbe mbali mbali kwa Zari kupitia
mtandao, hata hivyo Zari akiwa nchini Kenya May mwaka huu alisema hamjui
Ringtone kwani ana followers zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa
Instagram. Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa huenda Diamond na Zari
wamerudiana au kufanya hivyo hivi karibuni.
by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here