Zesco Yalazimishwa Sare Nyumbani, Mazembe Yaipiga Setif 4-1 Lubumbashi

0
4


Mshambuliaji wa Zesco United, Mkenya Jesse Were (kushoto) akijaribu kumpiga chenga mchezaji wa Mbabane Swallows jana

TIMU ya Zesco United jana imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani na Mbabane Swallows ya Swaziland katika mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia.
Haukuwa mwanzo mzuri kwa kocha George Lwandamina aliyerejea nyumbani mwezi uliopita kujiunga tena na Zesco akitokea Yanga SC kwa kulazimishwa sare hiyo na sasa wajibu wa kusimama imara kwenye mechi zijazo kuipa timu matokeo mazuri.
Beki Mkenya, David Owino alianza kuifungia Zesco United dakika ya 65, kabla ya Mangaliso Shongwe kuisawazishia Mbabane Swallows dakika ya 80.

Mechi nyingine za ufunguzi hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika MC Alger ililazimishwa sare ya 1-1 na Difaa Hassan El –Jadida ya Morocco Kundi B mjini Algiers huku Al Ahly SC ikilazimishwa sare ya 0-0 Esperance mjini Alexandria, Misri na Township Rollers ilishinda 1-0 dhidi ya KCCA mjini Gaborone, zote zikiwa mechi za Kundi A.
Mabingwa watetezi, Wydad Athletic Club, maarufu Wydad Casablanca ya Morocco walilazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Mamelodi Sundowns katika mchezo wa C Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini Camara Ibrahim alijifunga dakika ya tano, kabla ya kiungo Ismail El Haddad kuwasawazishia wageni dakika ya 20.
Mechi nyingine za jana; Horoya ilipata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya AS Togo-Port Kundi C mjini Lome, Primiero de Agosto ililazimishwa sare ya 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia nchini Angola katika mchezo wa Kundi D, wakati TP Mazembe iliicapa 4-1 ES Setif katika mchezo wa Kundi B mjini Lubumbashi.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA UFUNGUZI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Jumamosi Mei 5, 2018
Mamelodi Sundowns 1-1 Wydad Casablanca
AS Togo-Port 1-2 Horoya
1° de Agosto 1-1 Etoile du Sahel
TP Mazembe 4-1 ES Setif
ZESCO United 1-1 Mbabane Swallows
Ijumaa Mei 4, 2018
MC Alger 1-1 Difaa El Jadida
Al Ahly SC 0-0 Esperance
Township Rollers 1-0 KCCA

Credit: Bin Zubeiri

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here