Zama Za Yaya Toure Zimefikia Ukingoni Etihad , Guadiola Asema haya.. Kwaheri Toure

0
11
Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na
Manchester City, Yaya Toure hatimaye anaondoka City baada ya kuitumikia Klabu
hiyo kwa jumla ya Mechi 229 kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane 8. Toure
atacheza katika mchezo wa City dhidi ya Brighton katika ligi ya EPL, Pep
Guadiola aliliambia SPOTI TZ.

Mchezaji huyo kipenzi na mtaalamu wa kandanda
pale katikati ya uwanja ametoa mchango wake kiasi kidogo katika msimu huu, akiwa
na miaka 34 mkataba wake utaisha mwishoni mwa msimu huu wa 2017/2018
“Yaya hatakuwa nasi hapa City msimu ujao”
Guadiola alimwambia Mwandishi wetu, Guadiola alisema hayo wakati mabingwa hao
wa EPL wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Brighton utakaopigwa siku ya Juma
Pili. Na Yaya anatarajiwa kuwepo ndani ya dimba kama mchezo wake wa mwisho na
kuaga mashabiki wake wa Etihad
“Mchezo wetu na Brighton tutautumia kumpa
heshima anayostahili, moja kati ya njia nzuri na ya heshima kabisa mchezaji
anaweza kupewa kama namna ya kumuaga, tutakuwa tunadhamira ya kushinda kwaajili
ya Yaya na tutashinda kwaajili yake” aliongeza Mhispaniola huyo.
Toure alijiunga na City akitokea Barcelona,
kipindi ambacho Guadiola alikuwa anafundisha Barcelona kama Kocha mwaka 2010. Na
sehemu ya msimu uliopita alikosa michezo mingi baada ya kutokea kurushiana maneno
kwa Wakala wa Toure na Kocha wake huyo, Mhispaniola Guadiola.
Mchezaji huyo atakayefikisha umri wa miaka 35
mwezi huu, baadaye aliomba msamaha kwa kocha wake kutokana na kitendo cha
Wakala wake kutoleana maneno katika vyombo vya habari na Kocha wake huyo.
Msamaha huo ulimfanya Toure aongezewe mkataba wa mwaka mmoja.
Amecheza michezo 229 katika ligi ya EPL, kwa
kipindi cha miaka 8 nane, lakini amecheza michezo tisa 9 tu katika msimu huu.
Amefanikiwa kushinda mataji mawili, FA na mawili ya EPL.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here