YANGA: Tulieni bado tuna mechi 5

0
11
YANGA imewaambia mashabiki wao kwamba matokeo ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya USM Algiers yasiwapanikishe kwani bado wana michezo mitano mkononi.
Noel Mwandila ambaye ni Kocha wa viungo wa Yanga, ameliambia Gazeti moja la Algeria kwamba maji yalizidi unga kwenye mechi ya USM na hawakuwa na namna nyingine lakini bado ni mapema nafasi yao iko wazi.
Mwandila ambaye ni raia wa Zambia, alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuwa Kocha Mkuu wa kumalizia msimu wa Yanga lakini ghafla akaletwa Zahera Mwinyi ambaye ni Mkongomani.

“Tulikuwa tunajua tunakuja kucheza na timu kubwa kiasi gani na ndio maana tulijiandaa kadri tulivyoweza lakini uwezo wetu ndio uliishia pale na USM walistahili kushinda.
“Wachezaji ambao walikosekana kwenye kikosi cha kwanza waliathiri sana kiwango chetu na ndio maana matokeo yakawa vile, USM walitawala mchezo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
“ Silaumu wachezaji wangu, wamejitoa kadri ya uwezo wao na kila mmoja anapaswa kutambua hilo,”alisema Kocha huyo ambaye aliletwa Yanga na George Lwandamina ambaye amebwaga manyanga na kujiunga na Zesco ya Zambia.
“Bado tuna mechi tano mkononi lolote linaweza kutokea na bado uwezekano wa kufanya vizuri ni mkubwa,”alisisitiza Kocha huyo.
Credit: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here