Usm Alger Yaifanyia Kitu Mbaya Yanga, Yaipiga 4g

0
4
KLABU ya Yanga imeanza vibaya kaika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa USM Alger katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Julai 5 1962.
Katika mchezo huo mhimu kwa Klabu hiyo, Yanga iliwakosa nyota wake muhimu wakiwemo Ajibu, Chirwa na wengine huku ikikumbana na kichapo hicho kikali ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua hiyo.
Mabao ya USM Alger yametiwa kimiani na Oussama Darfalou katika dakika ya 4 ya mchezo, bao la pili likifungwa na Farouk Chafai dakika ya 33. Mpaka mapumziko Yanga walikuwa nyuma kwa mabao hayo mawili. Kipindi cha pili kilipoanza kilizidi kung’ara kwa wapinzani ambapo mnamo dakika ya 54 Mezziane alitikisa nyavu za Yanga na kuongeza bao la tatu.
Na zikiwa zimeongezwa dakika 4 mchezo kumalizika, Yanga ilifungwa tena bao la 4 na la mwisho na mchezaji Mohamed kwa njia ya penati, na kufanya matokeo hayo kwa ujumla yamalizike kwa wenyeji kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 4-0.
Credit: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here