Unamkumbuka Colina? Ndiye atakayechagua Mwamuzi wa Finali ya UEFA pale Kiev.

0
7
UNAMKUMBUKA yule mwamuzi wa Italia mwenye upara, Pierluigi Collina? Sasa ameachana na filimbi na ndiye amekuwa bosi wa waamuzi wa Uefa. Na yeye ndiye ambaye atampanga mwamuzi wa pambano la fainali kati ya Liverpool na Real Madrid pale Kiev.

Collina ndiye Mkuu wa Kamati ya Waamuzi ya Uefa na amekuwa akichunguza kila mechi kupitia kwa watu wake wa karibu na tayari anajua kwamba kumekuwa na utata mwingi katika mechi za Ligi ya mabingwa hivi karibuni.
Tayari homa ya pambano hilo litakalopigwa Mei 26 imezidi kupanda kutokana na timu zitakazocheza fainali hizo kuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka katika pande nyingi za dunia.
Waamuzi wenye viwango vya juu katika uchezeshaji wanatazamiwa kupitishwa katika mizani ya Collina lakini kwa mujibu wa kanuni mechi hiyo haitachezeshwa na waamuzi kutoka Hispania au England ambazo zimetoa timu zitakazocheza fainali hiyo. Mara nyingi kamati hiyo ya Collina huwa inachagua waamuzi wenye uzoefu zaidi na ambao wamefaya makosa machache zaidi katika msimu huu huku wengi kati yao wakitazamiwa kuwepo katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia. Waamuzi ambao wanatajwa kuwa katika orodha fupi ya kuweza kuchezesha pamoja hilo ni pamoja na Bjorn Kuipers wa Uholanzi, Damir Skomina wa Slovenia, Felix Brych wa Ujerumani, Jonas Eriksson wa Sweden, Clement Turpin wa Ufaransa na Cüneyt Çakir wa Uturuki. Hata hivyo, Cakir alisababisha utata katika pambano la Real Madrid dhidi ya Bayern Munich ambapo anashutumiwa kwa kutoipa penalti Bayern Munich wakati mlinzi wa Madrid, Marcelo alipoonekana kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Waamuzi wengi wamekidhi vigezo lakini Collina, ambaye ni mwamuzi maarufu wa zamani kutoka Italia ndiye ambaye atakuwa na kauli ya mwisho kuhusu nani achezeshe pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu.
Hata hivyo, nchini Italia Collina amelaumiwa na Rais wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli kwa kushindwa kuruhusu matumizi ya teknolojia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya huku akimlaumu pia mwamuzi huyo kwa kuzikandamiza klabu za Italia katika michuano ya Ulaya.
“Inabidi tuwe wapole na kupima suala hili. Nimeona kuna nchi nyingi zinatumia VAR na nimeona kuna matukio ambayo yanakwenda dhidi ya timu za Italia hivi karibuni. Rafu dhidi ya Cuadrado, Milan dhidi ya Arsenal, na Juventus dhidi ya Real Madrid.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here