Ukimya wangu ulisababishwa na msiba – Nisher

0
3
Mtayarishaji wa video za muziki, Nisher amefunguka kwa kuwaomba radhi
mashabiki wake kutokana na ukimya wa mwezi mmoja ambao alikuwa nao.

Nisher amedai matatizo ya msiba wa babu yake yamesababisha ashindwe
kufanya baadhi ya mambo pamoja na kukaa mbali na mashabiki wake.
Director huyo ameandika, “Siku 14 zilizo pita zimekua siku Ngumu sana
kwangu na ninachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabik wangu na wadau
wote mnao ni support nimeshindwa kabisa hata kupost wala kua karibu na
simu yangu kutokana na kwamba Nilifiwa na Babu yangu mzaa baba (mwanzo
KUSHOTO) ikanilazimu kuacha kila kitu nlichokua na fanya Dar (Maana mimi
ni Mtoto wa Kwanza kwetu) na kuja Arusha Kwaajili yakua karibu na
Familia lakini zaidi sana Baba Yangu (KATIKATI) Ambaye siku chache kabla
ya birthday yake alifiwa na baba yake mzazi…. Hii imenigusa sana na
Familia zetu pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakaribu na
imetukutanisha pamoja na kutufanya kua karibu zaidi katika kipindi hiki
kigumu. Ijapokua Babu alifariki katika uzee mwema Bado tunazikumbuka
Busara zake na Maneno yake ya Hekima na jinsi alivyo kua akipenda kila
mtu awe na Umoja na Mshikamano. Tutakukumbuka sana Mzee wetu Lala kwa
Amani. Naomba radhi sana Mashabik na wadau wangu wote kwa Delay zozote
zilizo/zinazo/zitakazo jitokeza katika kipindi hiki kigumu, na nashukuru
kwa privacy yenu pia.! #rip
Chanzo: Bongo 5

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here