Tetesi za Soka Barani Ulaya leo Jumatatu 07/05/2018

0
13
Meneja wa Manchester united Jose Mourinho amekubali mpango wa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kutoka Manchester United kuelekea Juventus msimu huu wa joto (Tuttosport, via Daily Express)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kuwa na matamanio ya mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele,aliyejiunga na mabingwa wa Ulaya na Uhispania, Barcelona( Catalan giants) kwa kitita cha £135m msimu uliopita, iwapo kiungo huyo mwenye wa umri wa miaka 20 atapatikana. (Sun)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic amesisitiza kwamba Manchester United haina makubaliano yoyote ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa kutoka Serbia. (Manchester Evening News)
Liverpool imepinga ripoti kutoka Ufaransa kwamba ilikuwa imekubali mkataba wa kumsajili nahodha wa Lyon Nabil Fekir. (Liverpool Echo)
Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri, ambaye amehusishwa kujiunga na klabu ya Chelsea amemwambia rais wa Napoli kumpiga kalamu iwapo hafurahishwi na kazi yake. (Daily Mirror)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema atawapatia medali yake ya kwanza wa ushindi alioupata kwa ligi ya Premia kwa watoto wake wakati anapotarajia kung’ara zaidi na klabu hiyo. (Manchester Evening News)
Meneja anayeiaga Arsenal Arsene Wenger ameonekana akiombwa tai yake na shabiki mchanga katika mechi ya fainali ya nyumbani na alikubali bila pingamizi yoyote. (London Evening Standard)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amemuonya Mohamed Salah aepukane na mtindo wa kujiangusha baada ya mshambuliaji huyo raia wa Misri kupewa kadi yake ya kwanza ya manjano msimu huu waliposhindwa na Chelsea 1-0. (Independent)
Meneja wa Watford Javi Gracia, amesema kwa kuimarisha kikosi chake Will Hudges , 23, anaweza kujipatia nafasi ya kujiunga na klabu ya Gareth Southgate ya England nakushiriki kwenye Kombe la Dunia. (Watford Observer)
Source: bbc swahili

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here