Steven Gerrard Awa Kocha Mkuu wa Timu hii kubwa Barani Ulaya

0
11
Steven Gerrard hatimaye amekabidhiwa Timu
kama kocha wake mkuu na hivyo kuanza kazi ya kuinoa timu hiyoa Meneja wake. Ni
Rangers ya Skotiland inayoshiriki katika ligi ya Scottish Premiership kwa
mkataba wa miaka Minne 4.
“Ninajisikia furaha na heshima kubwa sana
kuwa Kocha mkuu ajaye wa timu hii ya Rangers. Hakika hili siyo jambo dogo
kamwe. Nina heshima kubwa kwa timu hii na utamaduni wake” Alisema Gerrard.
“siwezi kabisa kusubiria kuanza kufanya kazi
hii kama kocha wa Rangers. Ninatarajia kuyajenga mafanikio makubwa katika klabu
hii, hasa nikiendeleza pale nilipoikuta.” Aliongeza Gerrard.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo alisema, “kutokea
mwanzon I kabisa mwa mazungumzo yetu na Gerrard, mazungumzo yetu yamekuwa yenye
mwitikio wa chanya kabisa na wenye dalili za kuzaa matunda. Na tunaamini kwamba
Gerrard ndiye mtu sahihi wa kuichukua Rangers kutoka hapa na kuiendeleza kwa
mafanikio makubwa zaidi” Alisema Dave King.
Gerrard ambaye uzoefu wake kama kocha ni ule
alioupata tu alipokuwa anafundisha kikosi cha Wadogo Liverpool yaani Under 18,
alikuwa ni Keptain mzuri na mwenye mafanikio katika siku zake kama mchezaji
muhimu wa Liver.
Gerrard kama kocha wa Rangers anakibarua
kizito hasa mbele ya timu bora kabisa zinazoshiriki ligi ya Scottish, mfano
kama Celtic. Lakini Gerrard anaamini anatosha kusimama mbele ya nguli wa
michezo ya mpira wa miguu kama kocha atakayekuwa na mafanikio akiwa na Rangers.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here