Steven Gerrard aanza rasmi maisha ya ukocha

0
1

Nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Rangers ya Scotland kwa mkataba wa miaka minne. 

Gerrard amechukua nafasi ya kocha Graeme Murty ambaye amesitishiwa mkataba wake wa muda mfupi aliopewa wakati akichukua mikoba ya Pedro Caixinha aliayefukuzwa kazi Oktoba mwaka jana.

Kiungo huyo mwenye heshima ya pekee kwenye klabu ya Liverpool atakuwa na kibarua cha kurejesha ushindani dhidi ya wapinzani wakuu wa Rangers nchini Scotland ambao ni Celtic.

Gerrard aliichezea Liverpool mechi 710 na kushinda mataji 9 katika miaka 19 aliyoichezea timu hiyo. Pia nyota huyo mwenye miaka 37 ameichezea timu ya taifa ya England mechi 114 na amewahi kuwa nahodha.

Mwenyekiti wa Rangers Dave King ameeleza kuwa wao kama klabu wana imani kubwa na Gerrard, kwani tangu wameanza maongezi naye amewaonesha ushirikiano mkubwa. Gerrard mwenyewe amesema amefurahia uteuzi huo na atajitahidi kulinda heshima ya klabu hiyo.
Credit: Sports Kitaa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here