Simba yajificha Dodoma kuhofia hujuma Singida

0
5

Dodoma. Simba katika kuhakikisha inatwaa ubingwa bila ya kupoteza mchezo wowote msimu huu imeamua kuweka kambi Dodoma ya muda ikijiandaa na mchezo wake dhidi ya Singida United utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.
Simba imewasili leo jijini Dodoma itakaa hapo hadi Ijumaa na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa timu hiyo, taratibu zote ikiwemo sehemu watakayofikia imeshaandaliwa pamoja na ulinzi wa kutosha kwa siku zote 2 watakazokaa Dodoma ili kusiwepo na hujuma yoyote.
Simba kabla ya mchezo dhidi ya Singida United inahitaji pointi 2, tu kutangaza ubingwa au matokeo ya sare ama kufungwa kwa Yanga leo Alhamisi dhidi ya Tanzania Prisons kutawapa taji hilo.
Credit: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here