Simba wanacheka kwa dharau

0
10

YANGA na Prisons walipokuwa wanacheza na Yanga, jopo la uongozi la Simba lilitulia na kufuatilia kila kilichokuwa kinaendelea na baada ya kusikia Wanajangwani wamepigwa mabao 2-0, Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, wakacheka kwa dharau.


Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara aliliambia Mwanaspoti kwamba wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, walitulia kusikiliza kinachojiri na baada ya dakika 90, wakabadili gia namna ya kuwavaa Singida.


“Kipigo walichokipata Yanga dhidi ya Prisons, kitawafanya wachezaji wetu waiendee Singida United, wakiwa na utulivu wa akili utakaowafanya wapate mabao mengi zaidi kama ilivyokuwa mechi ya mzunguko wa kwanza waliopigwa mabao 4-0.

“Jambo kubwa ni mashabiki wa Simba, waje kwa wingi siku ya kesho Jumamosi ili washuhudie tutakapokuwa tunakabidhiwa Kombe ni mwendo wa kuvaa suti kwa kwenda mbele, tumechukua ubingwa kwa haki na kinachofuata ni kujilinda tusifungwe ,” alisema.
Manara alisema wakati mechi ikiendelea kati ya Prisons na Yanga, alikuwa Dodoma akiwa amejifungia hotelini kwa maombi maalumu na baada ya kumalizika kwa dakika 90 akashukuru Mungu.


Kwa upande wa nahodha wa kikosi cha Yanga, Juma Abdul alisema kuvuliwa ubingwa na Simba kumemuumiza kutokana na mazoea waliokuwa nayo ya kushiriki michuano ya kimataifa.
“Yanga ni klabu kubwa kitendo cha kudondosha mataji mawili ya Kombe la FA na ligi kuu si kitu kidogo, viongozi wanapaswa kukaa chini na kubaini ambapo tuliangukia ili waweze kutengeza kwa badae,” alisema.

Lakini nahodha wa Prisons, Laurian Mpalile yeye alikuwa na furaha baada ya ushindi huo, akidai umewatoa sehemu moja kwenda nyingine na kuona wamewatendea haki mashabiki wao.
“Kuna raha kushinda nyumbani, hii imetuongezea hatua na nguvu ya kumaliza kishujaa mechi zilizosalia kwani tunapambania kumaliza nafasi tatu za juu,” alisema.
Credit: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here