Simba Bingwa Ligi Kuu Bara 2017/18, Bado Point 2 Tu!

0
8
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC.

 TIMU ya Simba imechapa Ndanda FC inayopambana isishuke daraja, bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufikisha pointi 65 katika msimamo wa ligi, lakini kinachowavutia watu zaidi ni kwamba timu hii ndiyo pekee katika msimamo huo ambao haijapoteza mechi.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya (kulia) akitokwa na mchezaji wa Ndanda FC.

 Yanga imeshapigwa mechi mbili, Azam im­epigwa tatu. Sasa Yanga ambayo ipo katika nafasi ya tatu, inahitaji zaidi ya miujiza ili iweze kuikamata Simba. Imeachwa pointi 17 ikiwa imebakiza mechi sita ambazo zina jumla ya pointi 18. Si rahisi.

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco (katikati) akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Ndanda

 Na hata kama Simba ikipoteza mechi zote zilizobaki, halafu Yanga ikashinda zote, zikalingana pointi, bado itawalazimu Yanga wafanye miujiza ya kufunga angalau zaidi ya mabao matatu katika kila mechi, kitu ambazo ni nadra kutokea.

John Bocco akimtoka mchezaji wa Ndanda

 Hakuna ubishi tena kwamba Simba imefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18 labda itokee miujiza isiyo ya kawaida. Kimahesabu, Simba wanatakiwa kupata sare mbili tu katika mechi zake tatu zilizobaki, hivyo unaweza kusema ina asilimia 98 za ubingwa.

 Na Simba hii itako­saje hizo sare mbili katika mechi zake tatu zilizobaki dhidi ya Singida, Kagera na Majimaji wakati hadi sasa imecheza jumla ya mechi 27 kwenye Ligi Kuu Bara bila kupoteza hata moja?

Makipa wa Simba wakishangilia ushindi baada ya mchezo dhidi ya Ndanda FC

Mdhamini mkuu wa Simba Mo Dewji akishangilia ushindi wa Klabu yake

Credit: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here