Real Madrid wagoma kufanya Guard Of Honour kwa Barcelona Leo! Hizi ndizo sababu zao

0
12
Barcelona wamenyakua taji la La Liga mwaka huu 2018, huku
wakiwa na michezo mkononi. Hivi sasa kilichopo katika mipango ya Barcelona ni
kulinda heshima na kuhakikisha kwamba wanamaliza michezo yao yote wakiwa
hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Ligi hiyo ya Uhispania.

Wanaokutana nao safari hii ni Real Madrid,ambao kwa desturi
ya soka wanapaswa kuwapa Barcelona gwaride la heshima “The guard of honour”  lakini Madrid wameapa kwa maisha yao kwamba
katu haitakuja kutokea kitu kama hicho eti wawape Barcelona gwaride la heshima.
Sababu hasa ya msingi haijaeleweka wazi lakini kumbukumbu
zinatupeleka mwaka jana December, ambapo Real Madrid walikuwa wameshinda taji
la klabu bingwa Duniani baada ya kuwafunga Gremio  goli 1-0 katika mchezo uliochezwa Abu Dhabi
ambapo Ronaldo alifunga goli hilo la ushindi kwa timu yake ya Madrid.
Hilo lilikuwa ni kombe la tano katika mwaka wa 2017 baada ya
kuwa tayari wameshinda Champions League, La Liga, Uefa Super Cup na Spanish
Super Cup.
Baada ya ushindi huo kule Abu Dhabi, Madrid walipaa anga
kurudi Uhispania ambako walipokelewa Kifalme na mashabiki wao na wahispaniola
kwa ujumla kasoro Barcelona tu! Baada ya kurudi walikuwa na mchezo dhidi ya
Barcelona wiki moja baadae.
Lakini katika mchezo huo ambao ndiyo ulikuwa wa kwanza toka
warudi kutoka Abu dhabi walikorudi wakiwa na heshima ya Dunia, Barcelona wao
waligoma kabisa kutambua heshima waliyonayo Madrid kana kwamba hawajui
kilichotokea , hivyo walikataa katakata kuwapa Madrid Gwaride la heshima katika
mchezo wao huo.
Kuna habari zinasambaa hapa Uhispania na Duniani kote kwamba
Madrid wameamua kwa umoja wao kwamba hawatawapa Barcelona Gwaride hilo ikiwa
ndiyo mchezo wa kwanza wa Barcelona toka walivyotwaa taji hilo la La Liga.
 Mchezo wa Barcelona
na Madrid unatarajiwa kufanyika Leo hii mnamo saa Tatu na dakika arobaini na tano
kwa masaa ya huko nyumbani Afrika Mashariki. 21:45. Muda huo ndiyo El Clasico
inatarajiwa kuisimamisha Dunia pale wanaume hawa watakapokuwa wanaziumiza nyasi
katika uwanja wa Camp Nou. Mchezo ambao Madrid wanataka kuharibu historia
inayotaka kuwekwa na Barca, ya kumaliza Ligi yao bila Kufungwa hata mchezo
mmoja.

SPOTI TZ, Lilimhoji
Kocha wa Barcelona Valverde, kwamba anadhani kutokupewa gwaride la heshima ni
kuikosea heshima Barcelona, alisema; “ mimi sifikirii hivyo”.

“Tumeshanyakua taji tayari, ndahani hilo ndilo la muhimu,
kama tutapewa gwaride au la si jambo la maana sana kulizungumzia mara kwa mara”
aliongeza kocha huyo ambaye amejitahidi sana kutokuongelea mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here