Ramos, Amtuhumu Suarez kwa tabia yake ya kujiangusha angusha.

0
6
Madrid, Hispania. Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos amemshutumu Luis Suarez, kwa kusema timu yake iligoma kusimamisha mchezo baada ya mshambuliaji huyo wa Barcelona kumia kwa sababu “tabia yake ilivyo”.

Mechi nyingine ya Clasico ilimalizika kwa sare 2-2, kwenye Uwanja wa Camp Nou jana Jumapili huku Barcelona ikiwa katika mstari mzuri wa kumaliza msimu wa LaLiga bila ya kufungwa.
Lakini Madrid walijikuta katika wakati mgumu kwa kukataa kutoa mpira nje baada ya Suarez kumia wakati walipokuwa wakijaribu kutafuta bao la ushindi.
Hata hivyo, Ramos hakujutia kitendo hicho kutokana na historia ya mshambuliaji huyo wa Uruguay alikuwa na lengo la kusimamisha mchezo.
“Yeyote ambaye angeumia na tungeona kuwa ameumia kweli, tungetoa mpira,” alisema Ramos.
“Tungefanya hivyo kwa heshima yake Lakini tunajua jinsi alivyo, aina yake ya uchezaji na jinsi tabia yake ilivyo, sikudhani ni muhimu kwetu kufanya hivyo kwake.”
Awali Madrid ilikataa kutoa gwaride la heshimu kwa Barca ambao tayari wametwaa ubingwa wa LaLiga msimu huu.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here