Rammy Galis “Mungu Anisaidie Niweze Kutoa HUKUMU”

0
6

Muigizaji Rammy Galis ni miongoni mwa watu waliokuwa karibu na Marehemu Agnes Waya “Masogange” na pia alishawahi kuwa mapenzini na Marehemu, kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika caption iliyotafsiriwa tofauti na mashabiki mbalimbali.

Hii ni kutokana na tetesi ambazo zimekuwa zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na waigizaji wa Bongo Movie na kusemekana kuwa wamekula hela za rambirambi ambazo zilitakiwa kuwafikia ndugu wa Marehemu Agness Masogange.

Rammy Galis ameandika “Namuomba mungu anisaidie ili niweze kutoa kile kitacho barikiwa katika kazi ya mkono wangu na wako [HUKUMU] , SANIA yupo kwa niaba yako ❤? #PumzikaSalama  #RipAgness#HUKUMU”

Aunty Ezekiel alijibu kile alichokiandika Rammy Galis “Wewe ulitoa shillingi ngapi kwenye huo msiba, punguzeni drama basi kwa mambo ya familia za watu tena wenye majonzi bado”

Credit: Udaku Specially

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here