Pluijm aapa kulipa kisasi kwa Simba

0
5
Kocha wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
KOCHA wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya Simba itakayopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, amesema kuwa lazima walipe kisasi kwa wapinzani wao hao.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumza na Spoti Jumatano, Pluijm alisema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwao kulipa kisasi kwa wapinzani wao hao waliowafunga mabao 4-0.
“Hii ni nafasi nzuri kwetu kulipa kisasi cha 4-0 tulipokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani hivyo na sisi tumejiandaa kulipa katika uwanja wetu wa nyumbani, kwa sasa sisi hatufikiri mechi yetu ya fainali na Mtibwa kwani ipo mbali, hivyo tunaangalia hii ya Simba,” alisema Pluijm.
Credit: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here