Nimepata cheti cha kidato cha nne, sina mpango wa kugombea Simba – Hassan Dalali

0
5
Related imageAliyekuwa
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali amesema kuwa licha ya
kuhitimu na kupata cheti cha kidato cha nne hana mpango wakuwania
uongozi ndani ya timu hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali

Mwenyekiti huyo wazamani wa Simba, Dalali aliachia ngazi mwaka 2010
baada ya harakati za uchaguzi kumtaka mgombea nafasi hiyo ya juu kuwa
angalau amefika kidato cha nne wakati yeye akiwa na elimu ya darasa la
saba.

Ile kanuni ilipokuja mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Simba na
wakati nafanya mabadiliko ya katiba nilikuwa Mwenyekiti wa mkutano ule
nilikubali lifanyike hilo jambo ambapo kwa mtu mwingine ingekuwa ngumu
sana.
Mimi nilijijua darasa langu la saba nikasema sawa hakuna tatizo tunakwenda na mabadiliko ya dunia sasa hivi.

Bila kukata tamaa akiwa na umri zaidi ya miaka 50, Dalali akaamua
kurudi darasani kuitafuta elimu hiyo na kueleza kuwa licha ya kuhitimu
na kupata cheti kinachomuwezesha kugombea uongozi wa juu ndani ya klabu
ya Simba lakini hana mpango huo.

Ni watu wachache sana au watu wazima wachache ambao
wanakubali kwenda darasani, kweli nimekwenda darasani nimesoma
nimemaliza na vyeti nimepata nashukuru Mungu ijapokuwa watu wanasema
sijapata ila nawaambia nimepata vyeti na nimefanya mitihani kupitia
baraza la mitihani la taifa lakini sinamawazo ya kugombea ndani ya klabu
ya Simba.

Dalali amesema pia licha ya Simba kuonyesha dalili za kutwaa ubingwa
msimu huu bila kufungwa mchezo hata mmoja lakini bado haiwezi kufikia
rekodi aliyoiweka akiwa kiongozi wa timu hiyo msimu wa mwak 2009/10.

Mwaka 2009/10 ndiyo tukachukua ubingwa bila ya kufungwa
tulishinda mechi zote na kutoka sare mechi mbili hata Azam FC nayo
ilichukua ubingwa bila ya kufungwa lakini ilitoka sare saba na kwa sasa
hivi timu yangu ya Simba imeshatoka sare mechi nane hatujamaliza michezo
minne hapo inamaana timu yoyote inayo taka kuvunja rekodi niliyoiweka
chini ya uwongozi wangu lazima itoke sare moja tu kwahiyo rekodi yangu
bado inakwenda tu ni kwamba haijavunjwa.

Hassan Dalali alichukua kijiti cha uongozi wa klabu ya Simba mwaka
2006 baada ya mgogoro wa kiutawala uliyoikumba timu hiyo kwa wakati huo.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here