Ndoa ya Msanii Stamina, Yaisimamisha Morogoro.

0
12
Mei 05, 2018 imekuwa ni siku ya faraja kwa mwanamuziki wa Hipi Hop Bonavetura Kibogo ‘Stamina’ baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu ajulikanaye kwa jina la Veronica mwenye asili ya Rwanda.
Shamrashamra zilitawala katika mji kasoro bahari, baada ya Stamina na Veronica kuingia katika Kanisa la Mtakatifu Consolata liliopo SUA mjini humo baada ya kwenda kufunga ndoa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mastaa ambao ni Roma Mkatoliki ambaye ndio alikuwa msimamizi wa harusi akiwa na mkewe, Ben Pol, Young Killer, Afande Sele.
Stamina aingia ukumbini akiimba
Pamoja na matukio mbalimbali kufanyika katika harusi hiyo,tukio ambalo lilifurahisha watu waliohudhuria katika ukumbi  wa Artubell uliopo Modeco mjini Morogoro, ni pamoja na Stamina kuingia ukumbini akiwa anaimba na mkewe wimbo wake mpya wa ‘Love me’ alioshirikiana na Maua Sama.
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here