Nay atoboa siri ya ukimya wake

0
11
BAADA ya kuwa kimya tofauti na ilivyokuwa zamani kila kukicha skendo, staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kutoboa siri ya ukimya wake.
Akichonga na Risasi Vibes, Nay alisema kwa sasa ameamua kujitenga na skendo kwani anajiandaa kugombea urais mwaka 2020 japokuwa hawezi kuweka wazi atagombea kwa chama gani hivyo akaona ni vyema aachane na skendo zisizokuwa na maana.
“Nimeamua kutulia na kuachana na skendo zisizokuwa na maana kwa sababu nina mpango wa kugombea urais mwaka 2020 sasa nikiwa na skendo chafu zitaniharibia,” alisema Nay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here