Mzee Yusuph Ameapa kulipua bomu hili ndani ya siku hizi Tatu.

0
3

Aliyewahi kuwa mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amefunguka na kusema kuwa hazitapita siku tatu lazima alipue bomu.

Mzee Yussuf amesema hayo baada ya moja ya mtu ambaye alifahamiana naye kwa masuala ya kidini lakini baadae amekuja kumbadilikia jambo ambalo amesema sasa limempa mafunzo ila lazima aliweke sawa ndani ya siku tatu hizi.

“Kinachouma ni pale Muislamu mweenzio kukujia kidini kisha kukugeukia mpaka unajiuliza huyu alikuja kwa ajili ya urafiki wa kidini lakini leo anakuulizaa na kukuambia maneno mpaka unajiuliza karitadi kwani? Kiuhalisia si kila mtu wa kumuamini na kuna watu huwezi kumjua mpaka uishi nae mda mrefu kidogo ili umsome na wengine washenzi mpaka huamini kama ni yeye lakini humjui ila mpaka ukae nae. Kweli usimdharau usiyemjua na pia usimuamini usiyemjua”


Baada ya kauli hiyo watu wengi walianza kumpa pole Mzee Yussuf huku wengine wakitamani kujua jambo gani ambalo limempata mpaka kutoa kauli kama hiyo ambayo inaonyesha wazi kabisa kuwa kuna jambo halipo sawa, ndipo hapo aliposema kuwa lazima aliweke sawa jambo hilo ndani ya siku tatu hizi.

“Mtanielewa tu Insha Allah ngoja bomu lilipuke, labda Allah aniokoe lakini siku hizi tatu kutoka leo hesabu tu lazima niweke wazi” alisema Mzee Yussuf .

Source: Udaku special 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here