Mbwana Samatta awaonya Serengeti Boys kufuatia ushindi wao wa kombe la CECAFA

0
4

Image result for MBWANA SAMATTAMshambuliaji
wa Taifa Stars  na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amewaonya
vijana wa timu ya taifa ya mpira wa miguu waliochini ya miaka 17,
Serengeti Boys kwa kuwataka waache kubweteka kufuatia ushindi wa kombe
la CECAFA mwaka 2018.

Mbwana Samatta

Samatta amesema anaamini kuwa Shirikisho la soka nchini Tanzania
(TFF) limewaandalia vijana hao mazingira mazuri hivyo ni wao tu
kujitunza na kuongeza juhudi.
Tunamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa“ameandika Mbwana Samatta kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo kwa upande mwingine Samatta ametoa pongezi kwa Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA “Hongereni sana ‘Serengeti’ (u17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17“.

chanzo bongo5
by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here