Makala: Kolabo 8 za kimataifa zinazosubiriwa Bongo

0
11

Wasanii wa Bongo Flava wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaupeleka muziki huo nje ya nchi na duniani kwa ujumla.

Kufanya kazi na wasanii wa nchi nyingine ni njia moja wapo
wanayoitumia wasanii hao ili kufikisha muziki huo katika nchi hizo. Pia
wasanii hutumia njia hii kama sehemu ya wao kujitangaza zaidi.

Hapa tumekuletea kolabo ambazo wasanii wa Bongo waliweka wazi
kuzifanya na wasanii kutoka nchi mbali mbali lakini hadi sasa hazijatoka
ingawa zinatajibiriwa kuja kufanya vizuri kutokana na uzito wa wasanii
hao.

1. Alikiba X Yvonne Chaka Chaka

December 15, 2016 ilikuwa ni siku ya furaha kwa mashabiki wa Alikiba
mara baada ya muimbaji huyo mwenye sauti ya aina yake kuweka wazi kuwa
amefanya ngoma na msanii mkubwa na mkongwe Afrika, Yvonne Chaka Chaka.

Ilikuwa si stori ya kuchukulia poa kwa msanii wa Tanzania kufanya kazi
na Yvonne Chaka Chaka a.k.a Princess of Africa ambaye amekonga nyoyo za
mashabiki wake kwa kipindi cha miaka 29 sasa. Mashabiki wake wamechiziki
vilivyo na ngoma kama I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for
Freedom, Makoti, Motherland na nyinginezo kibao.

Siku hiyo Alikiba aliandika katika ukurasa wake wa Instagram; ‘It
was a great honor and pleasure to meet Mama Yvonne Chaka Chaka who I
have loved and admired all my life . Thank you for hosting us and
sharing your memories, advices and guidance. I am truly grateful and
looking forward to our project,”.

Kuanza hapo mashabiki wake wakawa wanangojea ngoma hiyo. July 6, 2017
katika mahojiano na XXL ya Clouds FM, Alikiba alisema wimbo huo upo
tayari lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu wimbo umefanyika tu na
kuotoa ila aliwahakikishia mashabiki wake kila wimbo utatoka kwa muda
wake.

2. Harmonize X Tyga

March mwaka huu boss wa label ya WCB, Diamond Platnumz ndio aliweka
wazi kuwa kuna kolabo inakuja kati ya Harmonize na Tyga kutokea nchini
Marekani.

“Kuna nyimbo kafanya na wasanii wa ndani na nje. Harmonize ana nyimbo
mpaka na Tyga, ana nyimbo Harmonize na Tyga amefanya,” alisema Diamond.

Licha ya Harmonize kufanya kolabo na Tyga, wasanii hao wajawahi
kuonana uso kwa uso, bali ni makubaliano ya menejiment za pande zote
mbili kisha wasanii hao wakafanya wimbo kwa mtindo wa kutumiana sauti.
Hilo alilieleza Harmonie wakati wa mahojiano na Radio Five.

Kukamilika kwa kolabo hiyo na kutoka kutamfanya Harmonize kuwa msanii
wa tatu kutoka WCB kufanya kazi na wasanii wakali kutoka Marekani mara
baada ya Diamond aliyefanya na Ne-Yo na Rick Ross, huku Rayvanny
akifanya na Jason Derulo.

3. Vanessa Mdee X Major Lazer

Si kufanya wimbo tu, Vanessa Mdee na kundi la watayarishaji wa muziki
kutokea Marekani, Major Lazer tayari walionekana location kwa ajili ya
ku-shoot video ya ngoma yao.

April 17, 2017 mara baada ya Vanessa kutoka ku-perform kwenye tamasha la
Gidi nchini Nigeria, ali-share picha katika ukurasa wake wa Instagram
zikionyesha wakiwa location na Major Lazer.

Hii ilikuwa ni stori moja ya kibabe sana katika Industry ya burudni
Bongo, kivipi?. Kundi la Major Lazer linaongozwa na Diplo ambaye ameweza
kutayarisha ngoma mbili katika albamu ya Beyonce, Lemonade. Tuachane na
hilo.

Katikati ya November 2017 Vanessa Mdee alifunguka kwanini hadi sasa
kolabo na Major Lazer haijatoka kwa kueleza kuwa kolabo hiyo ni ya kundi
hilo (Major Lazer), hivyo wao ndio wenye mamlaka ya kuamua lini itoke.

4. Alikiba X Davido

Hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa Alikiba na Davido wana ngoma waliyofanya pamoja ila hakuna aliweza kuthibitisha hilo.

Tatimaye July 2015 katika Red Carpet ya tuzo za MTV MAMA, Davido
akaamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi kwa kueleza kuwa kolabo na
Alikiba ipo na siku si nyingi itatoka.

“I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy,” alisema Davido.

Hata hivyo July 2017 Alikiba alikuja kukanusha taarifa hizo kwa
kueleza hakuna ngoma iliyofanyika ila kuna mipango ya kufanya endapo
muda utapatikana.

“Unajua wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu
lakini kiukweli hakijafanyika chochote ila plan zipo za kufanya na muda
tukiupata tutafanya ila sijajua ni lini,” alisema Alikiba.

Kwa maelezo ya Davido na Alikiba kuna uwekano wa kutokea chochote
kati yao, endapo ikiwa ndivyo basi tuhesaba hiyo ni hit song ya aina
yake.

5. Weusi X Sauti Sol

August 2015 kundi la Sauti Sol kutokea nchini Kenya lilikuwepo
Tanzania kwa ajili ya media tour, katika mahojiano na FNL ya EATV
waliweka wazi baadhi ya kolabo walizofanya na wasanii kutoka kwenye
Bongo Flava.

Wasanii waliotajwa ni pamoja na Alikiba, Ommy Dimpoz, Weusi, Fid Q na
Vanessa Mdee, pia waligusia kolabo yao na Yemi Alade kutokea nchini
Nigeria.

Mwaka uliofuata, September 2016, rapper Joh Makini alithibitisha
kukamilika kwa kolabo hiyo na kinachosubiriwa ni vitu vichache ili
waweze kuitoa.

Hii nayo ni moja kolabo ambazo zinasubiriwa kwa hamu kutokana
inakutanisaha makundi mawili ya muziki. Kutoka kwa ngoma yao kutalifanya
kundi la Sauti Sol kuwa na kolabo mbili nchini Tanzani baada ya ile
waliyofanya na Alikiba na AY.

6. Izzo Bizness & Abela (The Amaizing) X Ycee

Mwishoni mwa August, 2017 Ycee kutokea nchini Nigeria alikuja kufanya
media tour Tanzania, ndipo alipokutana na Izzo Bizness na Abela Music
wanaounda kundi la The Amazing.

Kukutana kwao haikuwa bure bali waliingia studio na kurekodi ngoma ambao ulisimamiwa na producer Abba.

February, 2018 katika mahojiano na Bongo5 Izzo Bizness alisema
kinachokwamisha kolabo hiyo kutoka ni ku-shoot video pekee ila
wameshawasiliana na meneja wa msanii huyo na kuna hatua fulani
wamefikia.

7. Rosa Ree X Emtee

Rosa Ree ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Marathon’
aliyomshirikisha Bill Nass, March 23, 2018 aliingia studio na Emtee
kutokea nchini Afrika kusini.

Kwa takwimu za mwaka 2015 Emtee ni miongoni mwa marapa watatu
wanaochezwa zaidi nchini humo. Hivi karibu Rosa Ree aliweka wazi kuwa
video ya wimbo waliourekodi ipo tayari.

Kukamilika kwa ngoma hii na kutoka kutamfanya Rosa Ree kuwa na ngoma
tatu ambazo ameshirikisha marapa wenzake baada ya kufanya hivyo kwa
Khaligraph Jones na Bill Nass.

8. Rostam X Khaligraph Jones

Kundi la Rostam ambalo linaundwa na Roma na Stamina September 2017
walikuwa na media tour nchini Kenya ndipo walipokutana na Khaligraph
Jones.

Kukutana kwa hawa marapa watatu haikuwa bure bali waliingia studio na
kurekodi ngoma. April 2018 Rostam walirudi tena nchini kwa ajili ya
ku-shoot video ya ngoma hiyo.

Khaligraph Jones ambaye ameshafanya kolabo na wasanii wa Bongo kama
Young Killer, Rayvanny, Christian Bella, Chin Bees, Nikki Mbishi na Rosa
Ree, anatajwa na mtandao wa Africa Ranking kama rapper tisho zaidi
akifunga top 10 ya wale wakali kutoka Afrika.
chanzo-bongo 5

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here