Majeshi yamwagiwa vifaa vya michezo

0
5
Timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambazo zinajiandaa na mashindano ya majeshi yanayotarajiwa kuanza Mei 20, mwaka huu kwenye viwanja vya Uhuru na Twalipo jijini Dar es Saalam zimepewa vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 10 na Benki ya NMB

Timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambazo zinajiandaa na mashindano ya majeshi yanayotarajiwa kuanza Mei 20, mwaka huu kwenye viwanja vya Uhuru na Twalipo jijini Dar es Saalam zimepewa vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 10 na Benki ya NMB
Katika mashindano hayo timu za majeshi zitashindana kwenye soka, netiboli, riadha, ngumi, kulenga shaba na mpira wa mikono.
Meneja Mwandamizi na Mahusiano kwa Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko, akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo katika ofisi za NMB makao makuu juzi jijini Dar es Salaam, alisema msaada huo unatokana na uhusiano mzuri walionao na vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Alisema lengo la kusaidia vifaa hivyo ni kutambua umuhimu wa michezo kuibua vipaji na kulinda afya na ajira za vijana nchini.
“NMB tumeendelea kuwa na ushirikiano mzuri na majeshi ya JWTZ, hivyo hii ni mara ya tatu tunasaidiana nao katika masuala mbalimbali ya michezo,” alisema Mlaseko.
Naye Luteni Kanali, David Mziray, mbali na kushukuru kwa msaada huo, alisema watahakikisha wanavitumia vizuri ili kutimiza malengo ambayo yamejenga uhusiano na NMB.
Alisema vifaa hivyo vitaongeza chachu ya mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka na kuzitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa NMB wa kudhamini. Vifaa walivyopewa na NMB ni mipira ya michezo yote, jezi.
Credit: IPP MEdia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here