Madrid yaikatalia Barca makofi leo

0
8
KIKOSI cha Real Madrid hakitajipanga mstari na kuwapa heshima ya kuwapigia makofi wachezaji wa Barcelona wakati wakiingia uwanjani kwenye mechi ya La Liga itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Utamaduni huo wa kuwapigia makofi, ni heshima kubwa inayotolewa kwa timu ambayo imefanikiwa kutwaa ubingwa kabla ya ligi kumalizika Hispania.
Lakini nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos, hivi karibuni alitamka kuwa hawapo tayari kutoa heshima hiyo, na kwamba kikosi cha ‘Blaugrana’ hao kitaingia  Uwanja wa Camp Nou pasipo kukaribishwa kwa makofi kama ilivyo utamaduni wa Hispania.
Kufuatia Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga wiki iliyopita, mechi hiyo ya mwisho ya ‘El Clasico’ msimu huu, haiegemei zaidi katika kupata matokeo kwa ajili ya kujiimarisha katika nafasi nzuri kwenye msimamo, bali ni yakulinda heshima zaidi na rekodi. 
Barcelona itajisikia vibaya kwa kukosa heshima hiyo, lakini kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, mapema alipinga kikosi chake kutoa heshima hiyo kufuatia kudai kuwa wapinzani wao hao walikataa kuwapigia makofi wakati walipokutana Desemba mwaka jana baada ya Real kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Dunia. 
Zidane alisema, kupitia Gazeti la ​The Globe na  Mail: “Hatutawapigia makofi. Ni uamuzi wangu. Ukweli sielewe kuhusu utamaduni huu wa makofi, hivyo hatimaye hakitatokea tena.”
Real ina nafasi ya kuhakikisha kuwa Barcelona haimalizi msimu bila kupoteza, lakini jana ilikuwa ikisubiri kupata taarifa ya vipimo endapo Raphaël Varane na Isco watakuwa fiti kucheza mechi hiyo, kwa mujibu wa Gazeti la Marca. 
Aidha, Barcelona inatumai kumchezesha Andrés Iniesta, ambaye ameshathibitisha kuondoka mwishoni mwa msimu kufuatia Alhamisi Mhispania huyo kufanya mazoezi na wenzake. 
Credit: Ipp media

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here