KWASI: Haikuwa kazi rahisi kufika hapa!

0
11
Asante Kwasi
BEKI Mghana wa Simba, Asante Kwasi amefunguka kuwa, haikuwa kazi rahisi kwao kufikia hapo walipo mpaka sasa wanaona wa­naelekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kwasi amesema ushirikiano wao ndiyo ume­wa­fanya kuwa hapo licha ya kwamba walikum­bana na changamoto nyingi.
Mghana huyo am­baye kwa sasa ana mabao nane akiwa ndiye beki mwenye mabao mengi kwenye ligi hiyo msimu huu, amejiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea Lipuli FC.
Akizungumza na Spoti Juma­tano, Kwasi alisema kuwa ni vizuri na ni furaha kuona timu yake inafanya vyema na kuweza kufikia hatua ya kuelekea ubingwa jambo ambalo si rahisi.
“Nashukuru Mungu tunapambana na malengo yetu yanaen­da kutimia kwa kiasi kikubwa, ni furaha ku­weza kuona timu yako inatwaa ubingwa na kuweza kupata nafasi nzuri ya kuji­tan­gaza ki­mataifa, siyo kazi rahisi.
“Lakini ushiri­kiano wetu ndiyo umekuwa chachu ya mafanikio na kuweza kufika hapa tulipo siyo kazi rahisi changamoto ni nyingi lakini inabidi kupambana tu hakuna namna ili kuweza ku­timiza malengo ambayo tumejiwekea mpaka sasa,” alisema Kwasi.
Chanzo: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here