Kuwa na Ngozi Nyeupe Bila Kutumia Mkorogo

0
3

Wanawake wengi na baadhi ya wanaume wanatumia vipodozi vilivyo na kemikali ili waweze kuwa na ngozi nyeupe.


Ila leo nitakupa njia moja tu itakayoweza kukusaidia kuwa na rangi nyeupe bila kutumia kipodozi vyenye kemikali katika ngozi yako.


Ifuatayo ni njia itakayoweza kukusaidia.


Mahitaji:


1. Asali kijiko kimoja cha chai


2. Juisi (maji maji ya limau) kijiko kimoja cha chakula.


3. Maji ya uvuguvugu kiasi


Jinsi ya kutengeneza mchanganyiko wako:


1. Changanya juisi ya limau na asali katika chombo kimoja kisafi na uchanganye ukitumia uma au kijiko cha kawaida kwa dakika kadhaa.


Matumizi:


1. Osha uso vizuri ukitumia sabuni (kama unapata sabuni ya habbat soda inakuwa vizuri zaidi) na maji ya uvuguvugu kisha jifute na kitambaa kisafi.


2. Jipake mchanganyiko huo usoni na maeneo yote ya shingoni taratibu huku ukijipaka taratibu kwa dakika 10.


3. Osha uso kwa maji safi, mwisho jifute kwa taulo safi.


ZINGATIA: Fanya zoezi hili kwa wiki mara 1 mpaka mara 3.


Chanzo: Fadhil Paulo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here