Kocha wa zamani wa Yanga Chamangwana Afariki Dunia.

0
11
Blantyre, Malawi. Kocha wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Mmalawi Jack ‘Africa’ Chamangwana amefariki dunia jana nyumbao kwao Malawi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa kutoka nchini Malawi, zinasema kuwa, nyota huyo wa zamani wa soka nchini humo, aliaga dunia majira ya saa 2 usiku, katika hospitali ya Malawi Queen Elizabeth Central Hospital, iliyoko jijini Blantyre, alikokimbizwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu.
Kabla ya kufikwa na umauti, Chamangwana (61), alikuwa ni mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya Be Forward Wanderers.
Enzi za uhai wake, Chamangwana aliwahi kuinoa klabu ya Yanga na kuipa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, 2005 na 2006 wakati timu hiyo ikiwa na ‘ukata mkubwa’
Gwiji huyo anashika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji walioichezea timu ya taifa ya Malawi mechi nyingi baada ya kucheza michezo 133. 
Source: Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here