Klabu ya Samatta yatandikwa 5-0 Ligi Ya Ubelgiji

0
10
Mbwana Samatta akisikitika leo Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege

MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikichapwa mabao 5-0 na Standard Liege katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
Mabao ya Standard Liege katika mchezo huo yalifungwa na Mehdi Carcela dakika ya tisa na 88, Renaud Emond dakika ya 51, Edmilson Junior dakika ya 79 na Duje Cop dakika ya 83.
Samatta usiku huu amecheza mechi ya 86 tangu Nahodha huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
Kikosi cha Standard Liege kilikuwa: Ochoa, Agbo, Cimirot, Emond/Cop dk69, Carcela/Carlinhos dk88, Fai, Edmilson/Djenepop dk88, Luyindama, Cavanda, Laifis na Mpoku.
KRC Genk: Vukovic, Nastic, Dewaest, Aidoo, Maehle/Karelis dk80, Seck, Malinovskyi, Writers/Pozuelo dk55, Trossard, Buffel/Ndongala dk55 na Samatta.

Credit: BinZubeiry

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here