Kisa Diamond Platnumz, Msanii wa Pato Ranking Kuhamishia kazi zake Bongo

0
6
Msanii wa muziki Walid Ally (25), aliyepo chini ya lebo ya Amari Musiq, ametua rasmi nchini kuanza kufanya kazi zake.Walid yupo katika lebo hiyo inayomilikiwa na msanii wa Nigeria, Patoranking, ambaye ni kati ya wanamuziki wanaofanya vizuri barani Afrika na anga za kimataifa na
vibao alivyowahi kuitikisa navyo ni pamoja  My Woman, My Everything, God Over Everything, Make Am na Another Level.

Walid alitua usiku wa kuamkia leo, ambapo mbali na mambo mengine anatarajia kufanya shoo yake ya kwanza katika Hoteli ya Sleepway.
Msanii huyo alikulia Amsterdam, Uholanzi  tangu alipokuwa na umri wa miaka saba, na alikutana na Pantoracking mwaka jana katika shughuli zake za kimuziki.

Walid amesema sababu ya kuja nchini ni katika kuendelea kukuza muziki wake huku akilenga kufanya kazi na wasanii wa hapa na kuwapa raha Watanzania sehemu ambayo amezaliwa.

Mpaka sasa tayari ameshaachia vibao vitatu ikiwemo Dunia, Ni Wewe na Namna Gani alichofanya na Pantoranking.

Amesema katika maeneo yote anayofanyia kazi zake ikiwemo Uholanzi, Nigeria na Marekani wanautambua muziki wa Tanzania na kuahidi kutumia kipaji alichonacho kuitangaza lugha ya Kiswahili.
Pia amekiri kati ya wasanii wanaosikika huko na kuuliziwa ni Diamond, ambaye amesema amejitahidi kuitangaza Tanzania katika tasnia ya muziki.

Source:Mwanaspoti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here