Kinachotokea Yanga Kinaweza Kuwa Funzo Kwa Timu Nyingine

0
3

YANGA usiku wa kuamkia leo ilicheza mechi yake ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika bila ya nyota wake saba waliojiondoa kikosini kwa sababu mbalimbali.

Licha ya kila mchezaji kati ya hao saba kuwa na sababu ya kutokuwepo kikosini, taarifa zi­nasema wachezaji hao hawapo kikosini wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi ya nyu­ma.

Wachezaji hao saba ni mbali ya Amissi Tambwe na Donald Ngo­ma ambao ni majeruhi wa muda mrefu katika kikosi cha timu hiyo kongwe nchini ikiwa imean­zishwa katika miaka ya 1930.

Yanga imecheza na USM Alger bila ya nyota hao ambao kwa hakika wangeongeza kitu katika mchezo huo wa Kombe la Shirik­isho.

Suala la kudai kwa wachezaji wa Yanga halikuanza ghafla, bali ni kitu cha muda mrefu am­bacho kingeweza kutatuliwa ama kwa kuwaeleza ukweli wachezaji au kuita wadau wen­gine ili wasaidie.

Uongozi wa Yanga ungezun­gumza wazi kwamba hauna fedha za kuwalipa wachezaji hao kwa sasa na hata wache­zaji wangejua lakini ahadi isiyo­tekelezeka imekuwa fimbo ya mgomo baridi huu wa sasa.

Wachezaji hawa nao ni binada­mu wanaotegemewa na familia zao ambao soka ndiyo kila kitu kwao, sasa wasipopata msha­hara inaweza kuwa kikwazo cha kuendesha maisha yao.

Yanga ina wanachama wengi wenye fedha zao lakini kama uongozi unakaa kimya bila ya kuwafuata na kuwaeleza ukweli kuhusu nafasi ya klabu kiuchumi kamwe hawawezi kutoa cho­chote.

Kila mahali hali ya kifedha ni mbaya, hivyo ni jukumu la Yanga kuwa wakweli ili waweze kupa­ta msaada na hili ni somo kwa timu nyingine ambazo hazipendi kueleza ukweli wa mambo ka­tika timu zao.

Credit: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here