Joti aeleza ukweli kuhusu nyumba yake kuvunjwa

0
7

Related image
Hapo
jana May 03, 2018 Mchekeshaji Lucas Mhavile ‘Joti’ aligonga vichwa vya
habari mara baada ya kuwepo taarifa zilizodai kuwa nyumba yake iliyopo
Kibada, Kigamboni imevunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara, sasa Joti
ameeleza kilichotokea.

Akiongea na Clouds FM amesema si kweli kwamba nyumba yake imevunja bali
ni ukuta ndio umewekwa alama ya X ila amekiri kuwepo kwa zoezi hilo.
‘’Wanapanua barabara huku kwetu, lakini huo upanuzi wa barabara
haujahusiana na ubomoaji wa nyumba, wengi wanajua nyumba yangu ndio
inabomolewa lakini sivyo, kinachobomolewa ni ukuta tu,’’ amesema Joti.
Kwa mujibu wa Afisa Manispaa ya Kigamboni, Davidi Langa wakazi zaidi
ya 100 wa Kibada na Kisarawe wilayani Kigamboni nyumba zao zimewekea
alama ya X na kutakiwa kubomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara.
Chanzo cha tatizo ni Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi
iliyopima maeneo hayo, Tanroad walikuwa bado hawajaweka alama zao za
barabarani na viwanja hivyo ni vya muda mrefu, hivyo wamekuja kuweka
wakati vimeshaendelezwa, hata hivyo Mkuu wa wilaya hiyo, Hashim
Mgandilwa ameingilia kati suala hilo.
by richard@spoti.co.tz
Chanzo: Bongo 5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here