Huyu Ronaldo ana kazi moja tu… na hakuna namna inabidi tumpende tu!

0
17


Na Eston
        Hakuna
unachopewa wala utachopewa kila kitu kinatafutwa.‘’Kutoka sifuri mpaka kuwa
shujaa’’(from zero to hero) kilikuwa kibao moja matata kutoka kwa mwanadada
Sarah Connor mapema mwanzoni mwa mwaka 2005 na ilikuwa moja ya kazi nzuri
zilizowahi fanywa na Rob Tyger. Achana na maneno mengi yaliyokuwa ndani ya
wimbo huo, jina la wimbo huo lilitosha kuupa uzito wimbo huo masikioni mwa
watu.
        Ni
nini kwani watu wanachokiheshimu zaidi kutoka kwa mtu asiefaa kitu leo? ,ni
ushindi wa mafanikio yake ya kesho!!.Tangu mwanzo wa ulimwengu na kuendelea
imekuwa hivo na itaendelea kuwa hivo imekuwa njia pekee ya watu walionekana sio
kitu leo kujenga heshima yao kesho. Huna sababu ya kumchukia mtu wa ina hii
mimi binafsi ninawaheshimu sana watu wa aina hio bila kujali maisha yao kiujumla
ili mradi tu jana walikuwa sifuri mfukoni na leo ni mashujaa.
      Cristiano
Ronaldo Do Santos Aveiro ni mmoja ya watu hao ni aina ya watu ninao waheshimu sana
ni aina ya watu wale aliowaimba yule mwanadada wa kijerumani(Sarah Connor).
Ronaldo aliezaliwa na mama mpishi Maria Dolores na baba yake aliekuwa mtunzaa
bustani ya manispaa Jose Dinis Aveiro na mraibu wa pombe , maisha yake
yalionekana kutofaa kitu wakati wa udogo wake yalikuwa sifuri kweli kweli.
Ronaldo aliekulia katika familia ya kikatoliki alifikia hatua ya kuchangia
chumba kimoja na dada zake na kaka zake .
      Akiwa
katika ukuaji wake wazo pekee la ukombozi wake na familia yake lilikuwa soka. Kwa
kutambua hilo akiwa na miaka 12 alienda kufanya majaribio katika moja ya klabu
bora muda wote nchini ureno Sporting Cp. Majaribio ya siku 3 na hatimae
waliliridhia uwezo wake na kumsajili na mapema akajiunga na timu ndogo ya
vijana ,Ronaldo alieamini sana uwezo wake katika mpira wa miguu alifikia
makubaliano na mama yake ya kuacha shule na kujikita zaidi katika masuala ya
soka zaidi.
     Kwa
kweli huyu Ronaldo  tunaeomwongelea leo
ni habari nyingine kabisa kufikia hatua ya kupenya tiimu ya wakubwa ya  Sporting na kufanya vizuri na kutumia vema
kila nafasi iliotokea mbelea yake hasa mechi ya kirafiki dhidi ya klabu yake ya
baadae Manchester united ilibadili maisha yake kiujumla ulikuwa mwanzo wa
kumtoa kwenye sifuri kuelekea kuwa shujaa ni kama timu nzima ya Manchester
iliridhia usajili wake baada ya mechi yao ya kirafiki na Sporting kina
Ferdinand walikuwa wana kazi moja tu kumuuliza Fergueson alichoona toka kwa
Ronaldo Hawakuamini alikuwa ni kijana wa miaka 18 tu aliekuwa akiwanyanyasa
vile.
      Kuingia
united iliokuwa imara wakati huo na kupenya moja kwa moja hadi kikosi cha
kwanza kilichozungukwa na wakongwe kibao kama kina Louis Saha,Ruud Van
Nistelroy,Ryan Giggs na Diego Forlan halikuwa suala gumu kwa Ronaldo wakati
huo. Kuwa mchezaji bora wa dunia akiwa na miaka 22 tu bado halikuwa suala gumu
kwa Ronaldo na hatimae kutua kwenye viunga vya Bernabeu. Ronaldo huyu wa Madrid
ameshafanya kila kitu na bado ana kiu sana akiwa na umri wa miaka 33 bado tamaa
yake ni ile ile haridhiki hata kidogo. Unamuongelea mfungaji bora wa muda wote
ndani ya klabu ya Madrid , unamuongelea mchezaji alieipa Madrid makombe 14
ndani ya miaka 9 aliyokaa klabuni hapo Ronaldo ameionjesha Madrid kila aina ya
kombe iwe ni la liga(mara 2),copa del rey(mara 2),ligi ya mabingwa barani
ulaya(mara 3),kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu(mara 3) ,Uefa super cup(mara
2).
  
Unamuongelea mchezaji pekee duniani kufunga magoli zaidi ya 60 kwa kila
mwaka ndani ya miaka 4 mfululizo(2011-2014). Na mchezaji pekee kufunga magoli
50 au zaidi ndani ya miaka 7 mfululizo , kuwa mchezaji wa kwanza kuwa mfungaji
bora wa ulaya katika ligi mbili tofauti, mchezaji wa 1 kufikisha magoli 100
katika ligi ya mabingwa ulaya ,mchezaji wa 1 na pekee kufunga mechi zote katika
hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ulaya, mchezaji pekee kufunga katika
mashindano ya ulaya kwa ngazi za taifa 4 tofauti mfulilizo,hat-tricks nyingi
ligi ya mabingwa ulaya, pasi za mabao nyingi zaidi ligi ya mabingwa ulaya,
hat-tricks nyingi la liga, mchezaji wa kwanza kufikisha goli 300 kwa haraka
zaidi katika historia ya la liga, pasi nyingi za mabao la liga… yaani hatutamaliza
matukio yote ya  kijana huyu wa Madeira.
     Amefanya
mengi sana makubwa! Yanayotosha yeye kuitwa 
shujaa tena shujaa alieonekana kutofaa kitu udogoni mwake.Jambo la
kufurahisha zaidi hata leo akiwa na miaka 33 bado anafanya makubwa kuna kitu
kimoja Ronaldo anataka fanya msimu huu itakuwa ni adhabu  kwa 
kizazi kinachofata  mwanzoni
ilikuwa vigumu sana kuamini kuwa kuna timu ingeweza kutetea ubingwa wake wa ulaya
sasa hilo sio jambo gumu tena Ronaldo anataka afanye hivyo kwa mara ya 3!!!
Kama Ronaldo ataweza kufanya hivi ni nani 
anaeweza kusimama na kukataa Madrid ndio timu bora karibu Muongo mzima?
Ni nani anaeweza kuendelea kutafuta dosari yoyote ndani ya mchezaji huyu? Na
bado akasimama na kusema yeye ni mpenzi wa kweli wa soka na sio mpenzi wa timu fulani
au mchezaji fulani na bado watu wakamuelewa? Hakuna na hakuna!! Sahau ushabiki
wote uliopo kati ya Cristian na Lionel na uruhusu moyo wako uongee , sahau
ubishoo wake wote Ronaldo na maisha yake ya matanuzi sana yanayoweza kukukera
mtazame Ronaldo wa ndani ya uwanja tu.
      Iliwahi
kufikia hatua madridista wote pale Bernabeu walinyanyuka walau kwa dakika moja
na wakampigia makofi Ronaldinho Gaucho mioyo yao ilizishinda akili zao
wakasahau uhasimu mkubwa walio nao dhidi ya Barcelona walifanya tena miaka ya
karibuni dhidi ya Andres Lujani Iniesta na bado sijachoka kusubiri naamini kuna
siku watafanya hivyo tena mbele ya baba Thiago(Messi). Ndivyo soka lilivyo
wakati mwingine inabidi ufurahie kilicho bora bila kujali nani anafanya hivo,
Cristian nae msimu huu alipata heshima hio mbele ya wana Turin bao lake la
tikitaka liliwakosha sana wakasahau walikuwa nyuma kwa goli 2 wakasimama
wakampa heshima yake.
     Kama ubingwa utaanguka tena kwa vijana wa
zizou ruhusu moyo wako ufurahie hilo hata kwa muda mfupi, sio rahisi mimi na
wewe kuona timu nyingine itakayorudia kufanya hivo katika kipindi cha maisha
yetu. Kutoka sifuri mpaka kuwa shujaa una kila sababu ya kuvutiwa na upambanaji
wake Ronaldo ni kitia moyo na mfano bora kwa watoto wote wa ghetto wanapitia
msoto mkali leo. Ni kama anawaambia kesho yao inaweza kuwa bora sana, Ronaldo
ndio maana yote ya kibao cha Sarah Connor”from zero to hero”.
      
       

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here