Davido aweka wazi mahusiano yake na Chioma, ampa gari ya kifahari la 285m

0
13

Davido
sasa ameamua kuweka wazi mahusiano yake na Chioma. Msanii huyo ameweka
weka wazi hilo usiku wa jana katika sherehe ya kuzaliwa ya mrembo huyo
ambaye ametimiza miaka 23.

Mara kadhaa Davido amekuwa akikataa kuwa na mahusiano na mrembo huyo.
Katika sherehe hiyo Davido amemzawadia gari aina ya Porsche SUV yenye
thamani ya kiasi cha dola 125k ambapo ni zaidi ya shilini milioni 285 za
Kitanzania.

Lakini kubwa zaidi hit maker huyo wa Fall, kupitia Instagram, ameweka
video ya gari hilo wakati akimkabidhi mrembo huyo na kuandika ujumbe wa
kuthibitisha kuwa wao ni wapenzi.

“I give my baby ASSURANCE!!! I love you baby!! WE IN THIS 4 LIFE!!

BY richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here