Dalali: Sina mpango wa kugombea uongozi Simba

0
4

Hassan Dalali, Mwenyekiti wa zamani wa Simba ambaye ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea kwenye nafasi za uongozi ndani ya klabu hiyo.Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, maarufu kwa jina la ‘Field Marshal’ amesema hana mpango wa kuwania nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu hiyo.Dalali aliondoka kwenye nafasi hiyo mwaka 2010 baada ya kanuni mpya za uchaguzi zilizoweka sharti kwa mgombea uenyekiti wa klabu ya Simba kuwa na angalau elimu ya kidato cha nne.

Kanuni hizo zilimuweka kando Dalali aliyekuwa na elimu ya darasa la saba kwa wakati huo lakini bila kuona aibu akiwa na zaidi ya umri wa miaka 50, alirudi darasani kuitafuta elimu hiyo hadi akaipata.Akizungumza na Azam TV, Dalali amesema kuwa licha ya kuhitimu na kupata cheti kinachomuwezesha kugombea nafasi ya juu ya uongozi ndani ya Simba, bado hajafikiria kufanya hivyo kwa sasa.Akizungumzia mwenendo wa Simba msimu huu,
Credit :Presstz
 Dalali amesema licha kuonesha dalili za kutwaa ubingwa msimu huu bila kupoteza mchezo, bado wana kazi kubwa ya kufanya kufikia rekodi iliyowekwa na timu hiyo msimu wa 2009-2010 chini ya uongozi wake.Dalali aliingia madarakani mwaka 2006 baada ya mgogoro wa kiutawala ulioikumba klabu hiyo na anashikilia rekodi ya kuwa mwenyekiti pekee aliyevamiwa na mashabiki wa timu hiyo nyumbani kwake wakimtaka ajiuzulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here