Caster Semenya Ashinda Mbio Za Mita 1500 Kwa Wanawake.

0
9

Mwanariadha kutoka nchini Afrika Kusini Caster Semenya, ameweka rekodi kwa taifa lake kwa kushinda katika michuano ya awali ya mbio za msimu za mita 1500 kwa wanawake kwenye michuano ya Diamond League.
Semenya, pia alishinda tuzo ya dhahabu kwa nidhamu katika michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwezi Aprili , alitumia dakika tatu sekunde hamsini na tisa na ushee katika michuano inayofanyikia Doha.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27, ni mshindi mara mbili wa michuano ya Olympic mita 800, anaweza kuathiriwa na sheria mpya zinazowakabili wanariadha wa kike wenye homoni nyingi za kiume Semenya alipoulizwa juu ya ushindi huo wa mfululizo.
Semenya alisema: “Sizungumzi juu ya mambo ya kipuuzi.
Mwanariadha huyo kutoka nchini Afrika Kusini alizungumza mwishoni mwa wiki hii kwamba ushindi wake utawapa changamoto shirikisho la tidhaa ulimwenguni (IAAF) juu ya sheria mpya za mchezo huo.
Mkurugenzi wa shirikisho hilo la riadha ulimwenguni Bwana Coe amesema kuwa sheria, ambazo zitaathiri matukio ya kufuatilia kutoka mita 400 hadi kilomita, ni “sahihi kwa mchezo”.
Semenya anasema awali alinia kukimbia kwa kasi zaidi, lakini baadaye alipunguza kasi kiasi.
kila wakati ni kama ndoto kwangu kuweka rekodi kwa taifa langu nami nikaenedelea kujitahidi kadiri ya uwezo wangu wote. naamini tumefanikisha kile ambacho kimetuleta hapa.
Mkenya Nelly Jepkosgei alimaliza mbio hizo akiwa nafasi ya pili kwa kutumia saa nne na sekunde tisini na tisa., akifuatiwa na Mui Ethiopia Habitam Alemu aliyemaliza mbio hizo na kushika nafasi ya tatu.

Posted by Lebab

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here