Bella adaiwa kutonyonyesha, kushinda baa

0
5
LICHA ya kwamba ana mtoto mchanga ambaye alijifungua hivi karibuni, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ anadaiwa kuacha kunyonyesha na kwenda kushinda kwenye baa yake anayoimiliki.
Chanzo kilieleza kwamba, mwanamama huyo amekuwa akishinda siku nzima hadi usiku akitoa huduma baa huku akimwacha mtoto huyo mchanga, hali inayozua maswali kwa watu wake wa karibu kwamba, inakuwaje anamwacha, si anaweza kukosa malezi bora maana maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga hadi miezi sita?
Ili kupata ukweli wa madai hayo, Za Motomoto News ilimtafuta Bella ambaye alikiri kuwa kweli, baada ya kujifungua alikaa siku chache tu ndani kabla ya kuanza kazi ya kuhudumia kwenye baa yake ila amekuwa akienda kumnyonyesha mwanaye kila wakati.
“Unajua watu wanashindwa kuelewa, baa iko hapa karibu na ninapoishi, kwa hiyo natoka asubuhi kuja kusimamia na kuuza chakula na jioni pombe, nimekuwa nikirudi nyumbani mara kwa mara kumnyonyesha mtoto kwa kuwa sitaki kujilegeza na napenda kutafuta pesa na wateja wanahitaji kuniona ninawahudumia mimi,” alisema Bella.
Chanzo: IPP Media

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here