Barakah The Prince afunguka ishu ya kusaini WCB

0
7

Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amefunguka kuhusu tetesi za kujiunga na label wa WCB.

Muimbaji huyo ameiambia Rick Media kuwa WCB ni kama familia yake ila suala la kujiunga na label hiyo halina ukweli wowote.

“Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB
ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini,” amesema
Barakah.

“Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya
vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli,”
amesisitiza.

April 25, 2018 Dj wa Diamond Platnumz ‘Romy Jones/Rj The Dj’ aliachia
wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Bora Iwe akiwa amemshirikisha
Baraka The Prince.

Utakumbuka July 21, 2017 Baraka The Prince alitangaza kuondoka katika
label ya Rockstar4000 kwa kile alichodai kuna mambo hayapo sawa kati
yake na menejimenti hiyo.
by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here