Ambani ataka Yondani atimuliwe

0
5
STRAIKA wa zamani wa Yanga, Boniface Ambani ameshtushwa na taarifa za baadhi ya wachezaji wa timu yake hiyo ya zamani kuweka mgomo baridi wakishinikiza walipwe madeni yao.
Wachezaji saba wa Yanga hawakusafiri na timu hiyo Algeria ambako kesho Jumapili kikosi chao kitacheza mechi ya kwanza ya Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.
Nyota wa Yanga ambao hawakuondoka na timu ni Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshishimbi, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko, Beno Kakolanya, Obrey Chirwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Wachezaji hao kila mmoja ametoa udhuru kwa uongozi wengi wakidai wanaumwa na wengine kuwa na matatizo ya kifamilia, lakini gazeti hili linafahamu wapo kwenye mgomo baridi wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya nyuma.
Akizungumza kutoka Nairobi, Kenya, Ambani ambaye aliichezea Yanga kati ya mwaka 2008 hadi 2011, alisema; “Nasikia wachezaji wa Yanga wamegoma, hii si sawa japokuwa wana haki.
“Mchezaji anategemea soka ili aendeshe maisha yake lakini kugoma kwa wakati huu sidhani kama ni sahihi na kama ikibainika hawana sababu za msingi ni wazi watimuliwe.
“Watimuliwe sababu hawajui thamani ya kucheza mechi za Caf, huko wangejiuza na wanaonekana hawana uzalendo kwa timu, wangeenda kucheza halafu wadai baadaye, je, wakilipwa sasa wao wanaweza kuilipa Yanga kwa kukosekana katika timu?”
Ambani kwa misimu miwili aliyoichezea Yanga aliifungia mabao 42 huku lengo lake likiwa kufunga mabao 50.
Chanzo: Global Publishers

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here