Yanga yawatafuna wa Ethiopia 2:0 Chirwa akiwa jukwaani

0
9Kikosi cha Yanga kimeanza vema hatua ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaitta Dicha SC kutoka Ethiopia.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulianza kutikiswa nyavu zake kupitia Raphael Daudi, mapeka kwenye dakika ya 1.

Bao hilo moja lilidumu mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika ambapo Yanga walikuwa wanaongoza.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, Emmanuel Martin aliipatia tena Yanga bao la pili kwa njia ya kichwa na kudumu kwa dakika zote zilzokuwa zimesalia.

Mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho, Yanga 2-0 Wolaitta Dicha SC.

Mchezo wa marudiano utafanyika huko Ethiopia wiki moja baadaye.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here