Yanga yaiandalia pressure Simba

0
6Na George Mganga 

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Young Africans, leo asubuhi wamefanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Polisi Kurasini, tayari kwa kipute cha kesho dhidi ya Singida United.

Yanga itakuwa inaifukuzia Simba katika msimamo wa ligi ambayo imetangulia kwa alama 6 mbele huku ikiwa imecheza michezo 22 wakati Yanga ikiwa na 21.

Kama Yanga itapata ushindi kesho itakuwa imepunguza utofauti wa pointi na Simba kwa kuwa 3 badala ya 6 zilizopo hivi sasa. 

Mechi hiyo itakuwa ni harakati kwa Yanga kuendelea kuutetea ubingwa wake ambao imeutwaa mara tatu mfululizo huku pia ikiwa kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha FC utakaopigwa Aprili 18 2018 huko Ethiopia.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Emmanuel Martin pamoja na Rafel Daud.

Tayari Singida United walishawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo wa kesho utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here