Yanga wapewa mbinu hii kuimaliza Welayta Dicha ya Ethiopia

0
4
Kocha mkuu wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) adbulan Msoma ametoa ushauri wa bure kwa Yanga kuhusu  wapinzani wao Wolaitta Dicha kabla ya mechi yao ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika.
Msoma anaifahamu Wolaitta Dicha baada ya kucheza na timu yake msimu huu lakini Zimamoto iliondoshwa kwenye mashindano baada ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar kabla ya kufunga 1-0 kwenye mechi ya marudiano huko Ethiopia.
“Wolaitta Dicha kwa uzoefu wangu wa kufundisha timu zilizocheza mashindano ya Afrika, ni timu nyepesi kuliko timu zote nilizowahi kukutana nazo lakini maajabu ni kuona imefika hadi hatua hii.”
“Ni timu ambayo inategemea wachezaji wawili (nahodha wao ana rasta na kiungo mmoja anatumia mguu wa kushoto anavaa jezi namba 17) hao wanaweza kuwa tishio kwa timu yoyote.”
“Wachezaji wengine ni wa kawaida kabisa tena dhaifu kabisa, walinzi si wazuri kwa vichwa hawaangalii watu wanaangalia mpira ni suala la kufunga magoli tu, mie nimekosa magoli manne hapa Unguja na kule kwao nimegongesha mwamba mara mbili kwa sababu si wachezaji wanaojua kikamilifu wanachofanya uwanjani.”
“Ni wazuri kwa pasi fupifupi kwenye eneo la kiungo kwa hiyo kama mnafata mpira watawapita, lakini kama timu inawashambulia wanakuwa hawana la kufanya. Halafu ni timu dhaifu pembeni kwa hiyo nafasi ya timu kama Yanga naiona ni kubwa ikiwa watatumia mapungufu hayo.”
“Kiufundi waende mapema kwa sababu Ethiopia ipo juu na wale hawapo Addis Ababa wapo Awasa, wakifika Addis Ababa labda watalala siku moja halafu watasafiri kwa ndege kwa muda wa nusu saa wanafika kwenye huo mji wao.”
“Uwanja sio mzuri (pitch) kwa hiyo waende mapema kama siku nne au tatu wapate uzoefu wa hali ya hewa.”
Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here