Yanga kuwasili Dar leo na dozi ya Waethiopia

0
7


Kikosi cha Yanga kinatarajia kuwasili jijini Dar es Salaam leo tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC kutoka Ethiopia.

Yanga iliweka kambi mjini Morogoro kufanya maandalizi ya kuwawinda Waethiopia hao ambao tayari wameshawasili nchini tangu Jumanne ya wiki hii.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza utafanyika katika Uwanja wa Taifa kesho Jumamosi kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taarifa zilizotoka CAF zimeeleza kuwa Yanga itawakosa wachezaji Papy Kambamba, Kelvin Yondan, Said Makapu na Obrey Chirwa ambao wana kadi mbili za njano kwa kila mmoja.

Tayari uongozi huo umesema utafanya mawasiliano na CAF kupitia TFF ambapo umeeleza kwa rekodi zao unaonesha Yondani hakuwa na kadi mbili, bali alipata moja pekee

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here