WOLPER: Mimi ni shabiki wa Diamond tu! na Siyo WCB

0
1

Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuhusu ukaribu wake na label ya WCB kwa sasa.

Wiki iliyopita moja ya mtandao uliripoti kuwa muigizaji huyo kaeleza kuwa yeye si shabiki wa WCB bali Diamond.

Wolper amesema hilo halina ukweli wowote na kueleza kuwa watu wanaoelewa ukaribu wake na WCB hawawezi kutilia maanani hilo.

“Mtu akiangalia kauli kama hiyo atashangaa mimi siyo shabiki wa WCB, how ?, mimi nilijibu kutokana na swali, kwa hiyo watu wenye akili zao hawezi kufuatilia hivyo vitu” Wolper ameiambia Bongo5.

Wolper aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na muimbaji kutoka WCB, Harmonize ambaye pia alimshirikisha mrembo huyo katika video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Niambie. 

Chanzo: Udaku

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here