Vyombo vya habari italy vyamchana Olivier

0
5


Michael Oliver Mwamuzi kutoka Ashington, Northumberland, England, amekuwa gumzo kubwa hivi sasa mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Juventus dhidi ya Real Madrid.

Gumzo hilo limekuja kufuatia Oliver kutoa adhabu ya penati baada ya Lucas Vasquez kudondoshwa ndani ya eneo la hatari na kusababisha Mlinda Mlango wa Juventus, Gianluigi Buffon, kumtupia lawama Mwamuzi.

Kitendo cha Buffon kulalamika kilimfanya Mwamuzi Oliver kutoa kadi nyekundu kwa kipa huyo na kisha Juventus waliamua kufanya mabadiliko ya kutoa mchezaji mmoja na kumwingiza kipa Wojciech SzczÄ™sny.

Kufuatia tukio hilo mashabiki na wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia mengi kuhusiana
na Mwamuzi huyo.

Wapo wale wanaodhani kuwa Mwamuzi aliteleza kutoa tuta hilo ambalo lilikuwa ni zawadi kwa Ream Madrid iliyosonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali.

Mbali na hayo, vyombo vingi vya habari nchini Italy vimemtupia lawama Oliver kwa kusema kuwa aliboronga kulimudu pambano la jana.

Mengi yameandika kuwa maamuzi ya kutolewa penati hayakuwa sahihi huku yakieleza kuwa Mwamuzi alichemsha.

Moja ya gazeti lililomponda Mwamuzi Oliver linaitwa Corriere dello Sport.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here